title : CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI.
kiungo : CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI.
CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI.
Baadhi ya wanachama wa waliokuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la ukonga ikiwemo Kata ya Kitunda na kivule ambapo leo wametambulishwa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingungiti Omary Kumbilamoto (Katikati) akijisajili baada ya kuingia katika ukumbi uliopo Check point hotel jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutambulisha rasmi kwa wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala leo kimefanikiwa kuwatambulisha rasmi wanachama wapya waliojiunga na chama hicho kutoka vyama pinzani.
Baadhi ya wanachama hao walitambulisha na uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala ni pamoja aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mwita Waitara, Naibu Meya Manispaa ya Ilal na Diwani Kata ya Vingungiti Omary kumbilamoto pamoja na Mwenyekiti cha Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Mtwara.
Wanachana wengine ni baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Jimbo la Ukonga pamoja na wanachama wa CHADEMA ambapo sasa wameamua kujiunga na CCM.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyondaliwa na Uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kuwatambulisha wanachama hao, wamesema kuwa sababu ya msingi iliyosababisha kuhama kunatokana na utendaji bora wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Wanachama hao wamebainisha kuwa wamejipanga vyema kufanya kazi na Serikali na awamu ya tano kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala pamoja na kuhakikisha wanavibomoa vyama vinavyopinga maendeleo.
Akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala Mwita Waitara, amesema kuwa uongozi wa Chama cha CHADEMA umekuwa ukipinga juhudi za serikali ambapo kwa sasa inatekeleza kwa vitendo.
"Baada ya kuona yale ambayo nilitaka kuyafanya tayari CCM wanayafanya, na lengo ni kuleta maaendeleo ya wananchi, nimeona ni vizuri nikaongeza nguvu ili kufanikisha mipango yangu ambayo tayari inafanyiwa kazi" amesema Mhe. Waitara.
Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaosema watu wanaomia CCM wamenunuliwa kitu ambacho sio kweli, kwani kuhama kumetokana na kulizika na utendaji wa Rais wetu Dkt. Magufuli.
Agosti 7 mwaka huu aiyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti kwa tiketi ya CUF, Omary Kumbilamoto alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli.
“Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua hii ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumikia"
Alisema kuwa amefanya hivyo ili niendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo najivua ikiwemo kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla” amsema Kumbilamoto.
Alisema kuwa kwa sasa ataendelea na shughuli zake za kilimo mpaka pale atakapoamua kuwajulusha wananchi chama gani atachoamua kujiunga upya.
Hivyo makala CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI.
yaani makala yote CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/ccm-wilaya-ya-ilala-yawapokea-wanachama.html
0 Response to "CCM WILAYA YA ILALA YAWAPOKEA WANACHAMA WAPYA KUTOKA VYAMA PINZANI."
Post a Comment