title : Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil
kiungo : Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil
Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja ya kuendelezwa kwa kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Brazil itakayoratibu mashirikiano ya Kidiplomasia katika Nyanja za Kiuchumi, Historia na Maendeleo ikilenga kuimarisha ustawi wa wananchi wa pande hizo mbili.
Alisema Tanzania na Brazil zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni na Biashara unaopaswa kuendelezwa kwa kuzingatia kwamba ni Mataifa yanayofafana Kimaendeleo katika harakazi zao za kujiimarisha Kiuchumi.
Akizungumza na timu ya Wataalamu wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC Ofisini kwake Vuga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Kamisheni ya pamoja kati ya pande hizo mbili ipo lakini kinachohitajika kwa sasa ni ufuatiliaji wa malengo iliyoazimiwa kuyatekeleza.
Balozi Seif alisema Zanzibar kwa upande wake inaweza kufaidika na mpango huo kwa kujikita zaidi katika kufungua milango ya ushirikiano na Nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kwenye Sekta za Biashara, Taaluma katika masuala ya kukabiliana na Maafa pamoja na huduma za Afya.
Aliueleza ujumbe huo wa timu ya Wataalamu wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC likiongozwa na Bw. Fabio Webber Tagliari kwamba Zanzibar hivi sasa inaendelea kuimarisha Sekta ya Afya kwa kuvijengea uwezo zaidi vitengo vinavyosimamia huduma za Afya ya Mama na Mtoto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na timu ya Wataalamu wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC Ofisini kwake Vuga.
Kiongozi wa timu ya Wataalamu wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC Bw. Fabio Webber Tagliari kulia akiagana na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Mteule wa Brazil anayetarajiwa kufanya kazi zake Zanzibar mara baada ya kukamilisha kwa taratibu za Kidiplomasia.
Afisa wa Mahusiano ya Kimataifa wa ABD Bibi Layana Coasle Alves Kulia akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baara ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini kwake Vuga.
Hivyo makala Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil
yaani makala yote Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/balozi-seif-ali-iddi-akutana-na-timu-ya.html
0 Response to "Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil"
Post a Comment