title : BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
kiungo : BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala ametoa kiasi cha shilingi (milioni tano na laki sita ) 5,600,000/-kwa ajili ununuzi wa masanduku ya kubebea vifaa vya huduma ya kwanza (First Aid Kit) kwenye zahanati 10 za Halmashauri ya Missenyi,Masanduku hayo yakiwa na vitu muhimu vinavyohitajika kwa dharula mbalimbali.
Dr.Diodorus Buberwa Kamala amesema hayo alipofanya ziara katika Vituo vya Afya na zahanati kujionea changamoto na hali ya uwepo wa dawa na kuweka mikakati ya ufumbuzi katika huduma za Mama na Mtoto,Katika ziara hiyo ameongozana na Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Egidius Rwezaula .Amezitaja Zahanati zilizopewa (First Aid Kit) ni Kashanga, Buyango, Bugandika,Kitobo, Kanyigo,Minziro ,Kyaka,Kilimilile,Bugorora pamoja na Kakindo .
Bango la Zahanati ya Kashanga iliyopo Kata ya Bwanjai Wilayani Missenyi.
Balozi Kamala amepongeza hali ya utoaji na ubora wa huduma za afya Wilayani Missenyi na kuwapongeza MSD kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa huduma za Afya kupatikana .Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97).
Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula pichani kulia amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97)
Balozi Dr.Deodorus Kamala akiongea na wagonjwa waliofika katika ahanati ya Buyango pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Vituo vya Afya na Zahanati Wilayani Missenyi.
Hivyo makala BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
yaani makala yote BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/balozi-kamala-atembelea-vituo-vya-afya.html
0 Response to "BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO"
Post a Comment