title : WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO
kiungo : WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO
WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo ili kujadiliana masuala mbali mbali yanayozikabili wilaya zao. Waheshimiwa hawa waliweza kuangalia uzinduzi wa kitabu cha Dr. Reginald Mengi "I CAN, I MUST, I WILL".
Katika uzinduzi huo ambao Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alimpongeza Dkt. Regnald Mengi kwa maisha yake ya mfano ambapo hakukata tamaa licha ya changamoto nyingi kumkabili kiuchumi na kimaisha.
Mhe. Dkt. Magufuli alizungumzia pia namna ambavyo kuna watu ni wataalamu wa kukatisha tamaa wenzao. Hata Serikali inakutana na changamoto hizo za kukatishwa tamaa. Mfano ni Sera ya Elimu Bure, Ujenzi wa Reli ya SG, Mradi mkubwa wa Umeme wa Stiglers Gorge ambapo uliasisiwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere n.k
Aidha wakuu hao wa Wilaya walijadiliana namna ambavyo kama wanawake viongozi wanahakikisha wanawasaidia wanawake wenzao kujikwamua kutoka kwenye umasikini. Wanawake ni nguzo muhimu sana katika kuwaingiza Watanzania kwenye Uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kati. Nani asiyejua wachapa kazi wakubwa duniani kote ni Wanawake? Tatizo ni kuwa waliachwa nyuma kwa sababu mbalimbali ikiwemo Mfumo Dume, Sheria na Mila Kanzamizi hasa kwenye Umiliki wa Ardhi na njia nyingine za Uzalishaji Mali, Elimu, Afya, Ukosefu wa Mitaji na Mikopo nafuu n.k
Baada ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Magufuli kutangaza kwa nguvu zote Sera ya Viwanda na Uchumi wa Kati; wanawake wamekuwa na muitikio mkubwa sana. Matokeo ChanyA+ yanaonekana kila mahali.
Aidha waliweka mikakati mbalimbali ya kimaendeleo hasa kuangalia namna ambavyo wataweza kushirikiana Wilaya ya Gairo na Morogoro katika shughuli za maendeleo hasa kwa wanawake ili tufikie 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 SDG's Goal #5.
Wanawake ni nguzo muhimu ya kujenga uchumi imara Tanzania. Stay tuned; "The greater things are yet to come!." Ma DC wanawake Morogoro ni wawili tu na wanachapa kazi kwa pamoja kama sisters. Mhe. Regina Chonjo and Mhe. Siriel Mchembe (Iron ladies) katika ubora wao. Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (kulia) wakati alipomtembelea mapema jana ili kujadili maendeleo ya wilaya zao.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (kulia) wakati alipomtembelea mapema jana ili kujadili maendeleo ya wilaya zao.
Hivyo makala WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO
yaani makala yote WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wanawake-ni-nguzo-muhimu-ya-kujenga.html
0 Response to "WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA KUJENGA UCHUMI IMARA TANZANIA - DC WA MROGORO NA GAIRO"
Post a Comment