title : VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI
kiungo : VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI
VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI
Mwambawahabari
Vyombo vya habari nchini vimekubali ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda la kuendelea kutoa elimu ya utuzaji wa mazingira kikamilifu ili kuhakikisha Jiji linakuwa safi.
Vyombo hivyo vya habari ni pamoja na ITV, Radio One, Capital, TBC, Sahara Media, Uhuru Fm, Channel Ten, Azam, Clouds, ETV, EFm ambapo watendaji wakuu katika vyombo hivyo wamekubali
kutoa ushirikiano katika kufanisha kampeni ya usafi kwa Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mhe. Makonda amesema kuwa tayari ameongea na watendaji wa vyombo vya habari na wamekubali kuendelea kutoa elimu kwa jamii kikamilifu ili kufanikisha suala la usafi.
Mhe. Makonda amesema kuwa ameona ni vyema kutoa elimu kwanza kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kabla ya kuanza kuwakamata watu waochafua mazingira kwa makusudi.
"Usafi ni jambo ambalo linapaswa kupewa ushirikiano na kila mtu katika kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linakuwa safi muda wote" amesema Mhe. Makonda.
Ameeleza kuwa wakati umefika jiji la Dar es Salama linatakiwa kuwa safi muda wote, huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwake kama ikitokea katika maeneo yao kunatakata zimekaa muda mrefu bila kuzolewa.
Kwa upande wao watendaji wakuu wa vyombo vya habari wameaidi kuendelea kutoa elimu ya utuzaji wa mazingira kupitia vipindi mbalimbali katika redio na runinga ili kufanikisha kampeni ya usafi.
Hivyo makala VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI
yaani makala yote VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/vyombo-vya-habari-vyaungana-kusaidia.html
0 Response to "VYOMBO VYA HABARI VYAUNGANA KUSAIDIA KAMPENI YA USAFI"
Post a Comment