title : KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,
kiungo : KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,
KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,
Na Hamza Temba, Mbeya
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uchimbaji wa mchanga wa madini ya dhahabu (makinikia) ndani Hifadhi ya Msitu wa Palamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Amesema sheria za uhifadhi na mazingira hazihusu mtu yeyote kuchimba madini katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria bila ya kuwa na kibali maalum kutoka mamlaka husika.Ametoa onyo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwaoga, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya baada ya kukagua na kuona uharibifu mkubwa uliofanywa na wachimbaji hao kwenye hifadhi hiyo.
"Yeyote anayehitaji kuchimba madini kwenye maeneo ya hifadhi ni sharti afuate taratibu za kisheria ikiwepo kupewa kibali halali cha kufanya kazi hiyo, la sivyo tutakaowakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria" alisema Waziri Kigwangalla.
Ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee, Waziri huyo ameagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuweka kituo cha kudumu cha ulinzi katika eneo hilo ili kuwazuia wananchi watakaojitokeza kufanya shughuli hizo za uharibifu wa hifadhi hiyo.
Amesema, amebaini kuwa maeneo mengi makubwa ya uchimbaji wa madini katika wilaya hiyo yamemilikishwa matajiri wachache hali inayosababisha wananchi wa kawaida kukosa maeneo ya uchimbaji na hivyo kulazamika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala wakitembea mwendo wa mchakamchaka alipokuwa akikagua eneo la Hifadhi ya Msitu wa Palamela wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakikagua eneo lililoharibiwa kwa kuchimbwa mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mchanga wa dhahabu (makinikia) ambao umetaifishwa na Serikali baada ya kuchimbwa kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Amos Makala.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
Hivyo makala KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,
yaani makala yote KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA, mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kigwangalla-atoa-onyo-kali-kwa.html
0 Response to "KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,"
Post a Comment