TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA

TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA
kiungo : TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA

soma pia


TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA

Na Veronica Simba – Dodoma

Mtaalam Mwelekezi aliyeingia Mkataba na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kufanya Tathmini ya Mazingira (EIA) katika Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji Profesa Raphael Mwalyosi, amesema kuwa athari za kimazingira zilizobainika kuweza kutokea, zinaweza kuzuilika.

Ameyasema hayo leo, Juni 11, 2018 wakati akiwasilisha Tathmini hiyo ya Mazingira kwa Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zenye majukumu ya kutekeleza miundombinu wezeshi ya Mradi husika.

“Tathmini yetu imebainisha kuwa Mradi husika unaweza kutekelezwa pasipo shaka yoyote kwani athari zake kimazingira zinaweza kuzuilika. Muhimu ni kuweka mikakati ya kuzizuia,” alifafanua.

Uwasilishwaji wa Tathmini ya Mazingira kwa Kamati hiyo Tendaji, umefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati jijini Dodoma, ambapo ni moja ya hatua muhimu zinazoendelea kufanyika kabla ya kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi huo.

Wajumbe walioshiriki katika zoezi la uwasilishwaji wa Tathmini husika ni Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Maliasili na Utalii; Mambo ya Ndani ya Nchi, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Kilimo; Mifugo na Uvuvi pamoja na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Nyingine ni Wizara ya Fedha na Mipango; Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira; Ofisi ya Waziri Mkuu; Wizara ya Madini pamoja na Wizara ya Nishati, ambayo ndiyo yenye dhamana.

Aidha, wadau wengine walioshiriki ni Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Wakuu wa Taasisi za Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na TANESCO.
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zenye majukumu ya kutekeleza miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji, wakimsikiliza Mtaalam Mwelekezi, Prof Raphael Mwalyosi (aliyesimama), alipokuwa akiwasilisha Tathmini ya Mazingira ya Mradi husika, Juni 11, 2018 Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila, wakifuatilia uwasilishwaji wa Tathmini ya Mazingira ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji, Juni 11, 2018 Dodoma.


Hivyo makala TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA

yaani makala yote TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/tathmini-ya-mazingira-mradi-wa-umeme.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA"

Post a Comment