title : NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA
kiungo : NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA
NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA
Wengine 25 wajeruhiwa...Kamanda Polisi Mbeya alezea ajali ilivyotokea
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.
Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.
Amesema kutokana na mwendo mkali aliokuwa anaendesha dereva wa basi gari hiyo yenye namba T 755 BAB aina Scania alishindwa kumudu kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao
Amesema kuwa askari hao walikuwa wakitokea Igunga kwenda Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo mengine ya jeshi baada ya kumaliza mafunzo katika kambi ya Igunga.Amefafanua kuwa dereva wa gari hiyo naye amepoteza maisha na kwamba miili ya merehemu hao ipo chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Mbeya.
Amesema waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni askari 25 na wanne hali zao ni mbaya na sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya huku majeruhi waliobakia wakipatika matibabu katika hospitali ya JKT Mbeya kwani majeraha yao si makubwa.
Baadhi ya Askari wa JWTZ na JKT wakishriki kutoa msaada kwa Majeruhi waliopata ajali iliyotokea katika eneo la Kawetele mkoani Mbeya mapema leo mchana.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.
Hivyo makala NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA
yaani makala yote NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/newz-alertaskari-12-jkt-wafariki-dunia.html
0 Response to "NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA"
Post a Comment