title : TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA
kiungo : TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA
TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Rais wa Zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Leodegar Tenga amewataka uongozi wa klabu za Kandanda nchini kuwekeza katika soka la Vijana ili kupunguza matumizi ya kununua wachezaji wa kigeni.
Akizungumza na Globu ya jamii Michuzi, Tenga amesema kuwa klabu hizo zinatakiwa zitambue umuhimu wa kuwekeza kwenye kuandaa wachezaji wa baadae ilo kuweza kupunguza ununuaji wa wachezaji ambao kwa muda mwingine huwezi kupata mchezaji yule unayemtaka na ukimpata atakua na gharama kubwa.
"Ukitaka mafanikio lazima utengeneze mchezaji, klabu zetu zikiwa na mfumo huo wa uwekezaji kwa soka la vijana zitapunguza gharama kubwa wanazozipata kwa kununua wachezaji ambao kwa muda mwingine utapata mchezaji ambaye hujawahi kumuona uwezo wake na ukimtaka wa kiwango cha juu basi gharama zitakuwa kubwa," amesema Tenga.
Amesema, mafanikio yanakuja taratibu ila klabu zinatakiwa kukubali kwa mwaka mmoja au miwili kutengeneza timu bora kwa kuwaandaa wachezaji wako mwenyewe.
Tenga alitoa ushauri huo kwa klabu hizo baada ya kuona timu za Vijana zikiweza kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali nchini ikiwemo Serengeti Boys kurejea nchini wakiwa na kombe la CECAFA Challenge kwa vijana wenye umri wa miaka 17.
"Tumeona vijana wakipambana na kwa bahati nzuri mimi nilikuwepo Kule Burundi mashindano yalikofanyika, pamoja na changamoto za Mvua vijana waliweza kupambana na walicheza vizuri na kuibuka na ushindi huo ambao umeleta kombe nyumbani,"amesema Tenga.
" Baada ya miaka kadhaa tutakuwa na timu nzuri ya taifa kwani tutakuwa na wachezaji wengi waliokulia katika misingi mizuri ya kimpira".
Mbali na kuwa Rais wa TFF ,Tenga alicheza mpira kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Yanga miaka ya 80 sambamba na katibu mkuu wa Yanga wa sasa Charles Mkwasa.
Hivyo makala TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA
yaani makala yote TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/tenga-azitaka-klabu-za-ligi-kuu.html
0 Response to "TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA"
Post a Comment