MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI

MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI
kiungo : MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI

soma pia


MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI

*Katibu wa afya Dar, Wizara wazungumzia mafunzo waliyotoa kwa watumishi ili kuufanikisha mpango huo

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MPANGO wa matibabu ya afya kupitia utaratibu wa  Mfuko wa afya wa Jamii(CHF) iliyoboreshwa utakaoendana na utoaji wa kadi za bima kuanzia ngazi za vitongoji, unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Juni mwaka huu nchini kote.

Hatua hiyo inatokana na kuendelea kukamilika kwa mchakato wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa kada mbalimbali katika sekta ya afya ambao watahusika kwa namna moja au nyingine kusimamia mpango huo ambapo inaelezwa mpango huo utatoa fursa kwa wakazi wa majiji na halmashauri kunuifaka na CHF iliyoboreshwa ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanananchi wanakuwa kwenye mfumo wa kulipia matibabu kabla ya kuugua kwa kutumia kadi ya kadi za afya.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa Afya mkoa wa Dar es Salaam Sister Mathew wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa watumishi mbalimbali wa idara ya afya wakiwemo waganga  wakuu wa hospitali za wilaya pamoja na wataalamu katika mifumo ya utoaji wa  huduma hizo.Lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuhakikisha unafanikiwa.

Mathew amefafanua kwa kuzingatia umuhimu wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini  kote, Serikali ilifanya majaribio ya mpango huo katika hospitali zote zilizopo mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Morogoro na kutoa mafanikio, hatua iliyoilazimu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto kuja na mkakati huo kwa nchi nzima kupitia CHF iliyoboreshwa.

Amesisitiza wanaamini kuanza kwa utaratibu huo utawawezesha wananchi kupata kadi za afya kuanzia ngazi za zahanati zilizopo katika  vitongoji vyao na kwa asilimia kubwa utasaidia kuondoa changamoto kwa wananchi na watakuwa na uhakika wa kupata matibabu ya afya ya uhakika tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Mathew pamoja na mpango huo, kuanzia sasa huduma za utoaji wa kadi za matibabu kupitia utaratibu wa bima za CHF, utamwezesha mwananchi kupata matibabu kupitia vituo vyote vya afya tofauti na hapo awali ambapo utaratibu ulimtaka mwananchi kupata huduma kupitia kituo alichojiandikisha.
Mkufunzi Ally kebby akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya mpango wa utoaji huduma wa CHF iliyoboreshwa ambayo wameyatoa kwa watumishi mbalimbali wa sekta ya afya mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakipatiwa mafunzo kuhusu namna ya kutoa huduma za Afya kupitia Mpango wa Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)iliyoboreshwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI

yaani makala yote MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mpango-wa-matibabu-kupitia-chf.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI"

Post a Comment