title : Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo
kiungo : Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo
Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo
PICHA NA HABARI Za Freddy Macha

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel.
Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru. WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi, Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga....Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji.






Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax ni pia mwimbaji mahiri

Msanii wa mapishi Neema John aliyechangia kazi njema na Neema Kitilya.






Hivyo makala Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo
yaani makala yote Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/matukio-wasatu-ilivyovimba-birmingham.html
0 Response to "Matukio : WASATU ilivyovimba Birmingham, Uingereza kusaidia Vigoli Bongo"
Post a Comment