MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU
kiungo : MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

soma pia


MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

Mashindano maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia kuwavutia mashabiki wengi  wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote wa mbio hizo.

Katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’ ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo. 

Baada ya majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.

Tofauti na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae  kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa  mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.
Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.




Hivyo makala MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

yaani makala yote MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mashindano-ya-hisani-ya-mbio-za-mbuzi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU"

Post a Comment