MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2

MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2
kiungo : MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2

soma pia


MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2

Na Octavian Kimario
Mapato yanayotokana na utalii yameongezela kutoka Dola za Marekani Bil. 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 2.2 mwaka 2017 ambapo ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi A. Kigwangalla alipokuwa akifungua Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018.

" Wote tunaelewa ya kuwa Utalii ni moja wapo ya sekta zinazokua kwa kasi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kupunguza umasikini wa kipato. Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings)," alisema Dkt. Kigwangalla.

Aidha amesema, mafanikio ya Sekta ya Utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali  kutekeleza Sera hiyo kwa ushirikiano na wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji.

Dkt. Kigwangalla ametaja masuala ambayo yametiliwa mkazo katika  Sera hiyo kuwa ni pamoja na Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wote wa utalii katika kuhifadhi rasilimali za utalii, kuendeleza rasilimali watu, kuimairisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa,  kuimarisha mnyororo wa thamani katika mazao ya utalii pamoja na kuongeza wigo wa mazao ya utalii (kama vile kuendeleza utalii wa fukwe na utalii wa mikutano).

Vile vile kuweka mkazo katika kutangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii kimataifa,  kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji,  pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani na kuendelea kusimamia viwango vya ubora wa huduma za malazi nchini.

" Mtakubaliana nami kuwa, leo tunayo kazi kubwa iliyopo mbele yetu, hivyo ni vema kuweka mawazo yetu kwa pamoja katika kipindi cha masaa machache yajayo na kuibuka na maboresho kwa ajili ya rasimu hii ya Sera kwa mustakabali wa sekta ya Utalii nchini," alifafanua Dkt. Kigwangalla.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
  Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakati alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
  Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakimsikiliza Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (hayupo pichani) alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Wadau wa Sekta ya Utalii na Washiriki wa Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakati alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2

yaani makala yote MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mapato-ya-utalii-yaongezeka-kutoka-dola.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2"

Post a Comment