title : MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE
kiungo : MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE
MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE
Na Hamza Temba-WMU-Songwe
Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo utafanya maadhimisho ya siku ya Kimondo cha Mbozi kwa mara ya kwanza katika historia kwenye Kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali, wilayani Mbozi kuanzia Juni 28 hadi 30 mwaka huu .
Maadhimisho hayo yataenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vimondo duniani ambayo yaliazimiwa kufanyika Juni 30 kila mwaka na kikao cha Umoja wa Mataifa cha tarehe 6 Desemba, 2016.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kiliazimia tarehe hiyo kuwa siku ya kuelimisha umma kuhusu elimu ya anga na mafanikio ya tafiti mbalimbali yaliyopatikana kuhusu elimu hiyo, kutambua juhudi zilizofanyika, kuweka sheria za kimataifa na kutoa tahadhari juu ya athari zinazoweza kutokea endapo dunia itafanya uharibifu juu ya anga.
Taarifa hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Herman Tesha wakati akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maadhimisho hayo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye alitembelea kituo hicho kwa ajili ya kukagua shughuli za maandalizi.
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutangaza Kimondo kama kivutio muhimu cha utalii mkoani Songwe pamoja na vivutio vingine vya mkoa huo kwa ujumla ili kutoa fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya utalii mkoani humo.
Amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na kongamano la uwekezaji na sayansi ya vimondo, maonesho ya malikale, maonesho ya kiutamaduni, mashindano ya riadha (Kimondo Marathon), mashindano ya netiboli na mpira wa miguu (Kimondo Ligi).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiangalia Kimondo cha Mbozi alipotembelea kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua mpaka wa eneo la kituo cha kimondo na vijiji jirani alipotembelea kituo hicho cha utalii katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua kituo cha taarifa cha Kimondo cha Mbozi alipotembelea kituo hicho cha utalii katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha kimondo katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Nyuma yao ni jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake umekamilika.
Hivyo makala MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE
yaani makala yote MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/madhimisho-ya-kimondo-cha-mbozi_14.html
0 Response to "MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE"
Post a Comment