title : BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA
kiungo : BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA
BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA
Balozi wa Ireland nchini Paul Sherlock leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kuona maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland.
Katika ziara hiyo Balozi Sherlock ameambatana na ujumbe wa watu saba wakiwemo wabunge watatu kutoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali nchini Ireland. Ujumbe huo umetembelea jengo la watoto katika wodi ya watoto wenye Saratani na jengo la wazazi namba moja wodi ya watoto wachanga .
Balozi huyo akipatiwa maelezo kuhusu watoto wenye Saratani Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tumaini la Maisha (TLM) Dkt. Trish Scanlan amesema TLM wanashirikiana na MNH kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto wenye saratani kwa kuwapatia matibabu stahiki.
Akifafanua amesema ugonjwa wa Saratani kwa watoto ambao unaongoza nchini ni Saratani ya damu, jicho , figo pamoja na saratani ya matezi.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock akitambulisha ujumbe wa watu saba wakiwamo wabunge watatu wa Kamati ya Hesabu za Serikali ya Ireland kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru alipotembelea hospitali hiyo leo. Balozi huyo ameitembelea MNH leo ili kuona na kupatiwa maelezo ya miradi mbalimbali ya afya inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland. Waliosimama nyuma ya Balozi huyo ni watumishi wa MNH wakiwamo wakurugenzi, wakuu wa idara na vitengo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na ujumbe wa watu hao leo.
Mkuu wa Kitengo cha Saratani kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Rehema Laiti (kulia) akiwaeleza wabunge wa kamati hiyo jinsi wanavyowahudumia watoto wenye matatizo ya saratani waliolazwa kwenye hospitali hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha, Dkt. Trish Scanlan akieleza taasisi yake inavyotoa huduma ya tiba kwa watoto wenye saratani ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock katika hospitali hiyo.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock (kushoto) na ujumbe wake wakiwa picha ya pamoja na watendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hivyo makala BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA
yaani makala yote BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/balozi-wa-ireland-asifu-muhimbili-kwa.html
0 Response to "BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA"
Post a Comment