title : Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman
kiungo : Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman
Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi alisema uwepo wa Jumla la Ajabu liliopo Forodhani Mji Mkongwe maarufu {Beit Al Ajaib}utaendelea kuwa utambulisho wa Zanzibar Kimataifa katika masuala ya Kihistoria na Utamaduni.
Alisema Jengo hilo Maarufu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Dunia tokea Karne ya 17 linastahiki kufanyiwa matengenezo makubwa ili kulirejeshea hadhi yake ya kawaida na Oman tayari imeshajitolea kugharamia matengenezo hayo.
Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyeambatana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Bwana Hamud Al Has alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Salum alisema hatua ya Serikali ya Oman kujitolea gharama za Matengenezo ya Jumba hilo imekuja kutokana na Historia kubwa ya Uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Oman kwa Karne kadhaa zilizopita.
Alisema Historia ya pande hizo mbili zenye udugu wa Damu hasa katika masuala ya Utamaduni utaendelea kuwepo na kuimarishwa kwa faida ya Vizazi vya sasa na vile vitakavyokuja hapo baadae.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi Kulia akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. Katikati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Nyuma ya Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Hamud Al Has.
Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyenyanyua Mkono akielezea Mikakati ya Oman katika kuendeleza Uhusiano na Zanzibar wakati akizungumza na Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kutoka Kulia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza Kutoka Kulia akiishukuru Serikali ya Oman kwa misaada inayoendelea kutoa kwa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyevaa Kilemba akifafanua jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao na Balozi Seif. Kushoto ya Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Kulia ya Balozi Seif ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed. Picha na – OMPR – ZNZ.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman
yaani makala yote Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/balozi-seif-akutana-na-kufanya.html
0 Response to "Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman"
Post a Comment