TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL

TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL
kiungo : TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL

soma pia


TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL

Na Leah Mushi( Afrika Kusini)

“Embu jiulize ni namna gani shujaa wa taifa angejisikia pale ambapo amekaa mbele ya watu wa rika tofauti jinsia tofauti wenye mirengo tofauti ya kisiasa wote wakimsifia na kumshukuru kwa werevu wake wakulipigania taifa?”

Maneno ya Mama Graca Machel mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto wa Afrika akiongea mbele ya umati wa watu kutoka maeneo mbalimbali duniani waliofika kutoa salamu za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Winnie Mandela aliyefariki tarehe 2 Aprili 2018 nchini afrika kusini.

Winnie Madikizela-Mandela (81) alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo hali iliyopelekea kufungwa mara kadhaa mbali na kuendelea kupokea vitisho lakini aliendea kuwa mwanaharakati mpaka mauti yaliyomfika. 

Winnie Mandela ambaye kwa wengi anafahamika kama mama wa taifa la Afika Kusini pia alikuwa mke wa Nelson Mandela  kwa miaka 38 toka mwaka 1958 mpaka walipoachana mwaka 1996 na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Akiongea katika Msiba huo mama Graca Machel ambaye amekuwa akimuita Marehemu Winnie Mandela “dada mkubwa” amesema ni wakati sasa wa kuwaita mashujaa wa taifa na kuwashukuru wangali wakiwa hai kwakuwa hakuna ajuae kama wanasikia na kuona vile wanavyosifiwa wakati wa Misiba yao.

Pia amekemea tabia ya jamii kuwananga na kuwasema watoto wa wapigania uhuru kwakuwa wengi wao wamekosa miongozi na malezi bora ya wazazi kwakuwa wazazi wao walikuwa na ujasiri wa kuacha familia zao na kupigania taifa hivyo si sawa kuwasema na kuwanyooshea vidole badala yake waoneshe upendo zaidi kwao katika kile kilichofanywa na wazazi wao.

Kuhusu rambirambi na ahadi zinazotolewa misibani Mama Graca amewataka wananchi na wanasiasa kuacha maneno ya hadaa kwakuwa mengi yanayoahidiwa hayatekelezwi.

Akitolea mfano wa ahadi zilizotolewa wakati wa wa msiba wa Nelson Mandela miaka mitano iliyopita amesema “ kwasasa ukiangalia Afrika kusini mambo yamekuwa mabaya zaidi ya kipindi Mandela yuhai na hii inaonesha kiasi gani watu hawaishi ahadi zao walizoahidi na ndio jambo hata leo watu wengi wameahidi kuendeleza harakati za Winnie Mandela lakini nani anajua kama zitatekelezwa?”

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL

yaani makala yote TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tuwakumbuke-nakuwashukuru-mashujaa-wetu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL"

Post a Comment