title : TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU
kiungo : TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU
TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya tatu umeendelea kunufaisha wananchi wakiwemo wakazi wa kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima na Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoaniSimiyu.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango huo, Bibi. Rebecca Masunga kutoka Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi, amesema TASAF imemsaidia kutoka katika umaskini sasa anapata kipato kinachomwezesha kujikimu, kwa kuwa amelima ekari tatu za pamba, ekari moja ya mahindi, ana ng’ombe 14 na mbuzi wanne na amenunua plau kwa ajili ya kulimia.
“Nilikuwa maskini wa kutupwa , nilipoingia TASAF na kuanza kupokea zile elfu 36 nilikopa fedha nikalima nyanya ekari moja nikauza, nilipata shilingi laki sita nikanunua ng’ombe watatu wakakua; baadaye nikawauza nikapata milioni moja na laki tano nilinunua ng’ombe 14 ndiyo hao mnaowaona tunawachunga sasa” alisema Rebecca Masunga
“Tuna kikundi chetu ambacho tunaweka fedha zetu baadaye tunagawana, tukisha gawana tunaenda kuzalisha, tunalima nyanya, kabeji, pamba halafu tunauza; mpango wangu wa baadaye niwe na mtaji mkubwa na nijenge nyumba bora ” alisisitiza Bibi.Masunga.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakikagua shamba la pamba la mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga (mwenye kitambaa cheupe kichwani) wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akimpongeza mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi kwa kununua jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) kwa ajili ya kulimia, wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea na kuona nyumba ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Stella Masamaki wa Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi, wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Hivyo makala TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU
yaani makala yote TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tasaf-yaendelea-kuwanufaisha-wananchi.html
0 Response to "TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU"
Post a Comment