title : MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA
kiungo : MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA
MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali wakiongozwa na Rais mstaafu Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete wameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa (76) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mzee Mtopa amefariki dunia jana asubuhi ya Aprili 9 mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa ratiba ya maziko ya mzee Mtopa anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Kijijini kwake Nanjilinji wilayani Kilwa mkoani Lindi ambako leo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walijitokeza kumuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Mwili wa mzee huyo ulianza kuagwa saa mbili asubuhi na kuendelea hadi mchana hospitalini hapo.
Kabla ya kuaga mwili huo viongozi kadhaa akiwamo Mzee Mwinyi, mzee Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana walishiriki kwenye ibada iliyofanyika katika msikiti uliopo katika Hospitali hiyo ya Muhimbili.
Mbali ya viongozi hao walikuwepo viongozi wengine kadhaa ambapo kila mmoja aliyepata nafasi ya kumzungumzia Mtopa wamesema kifo chake ni pengo kwa CCM kwani alikuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele.
Baada ya kuagwa kwa mwili huo safari ya kuusafirisha mwili huo ilieneza kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Lindi.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu, Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa leo katika Mskiti wa Mhimbili , jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.
Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Dk.Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa mtoto wa marehemu wa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa mara baada ya kuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika viunga vya hospitali ta Taifa Muhimbili baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa.
Hivyo makala MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA
yaani makala yote MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mzee-mwinyi-kikwete-waongoza-mamia-ya.html
0 Response to "MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA"
Post a Comment