Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba

Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba
kiungo : Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba

soma pia


Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wenye thamani ya shilingi milioni kumi.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bi. Nuru Mhando amesema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote hivyo imeamua kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa msaada wa viti vya kubebea wagonjwa  na vipima joto vya kisasa .

‘’Kwa kutambua hilo mamlaka imeona ni vyema iunge mkono juhudi hizi katika wiki hii ambayo tupo kwenye shamrashamra za kuadhimisha miaka kumi na tatu tangu TPA ianzishwe, Aprili 15 ,2005, Mamlaka imeona ni vyema kusheherekea kumbukumbu hizi kwa kutoa mchango huu ili kusaidia wagonjwa katika jengo la watoto.

‘’Tunaamini msaada huu utasaidia kuhudumia watoto wengi kwa wakati mmoja na hivyo kutatua changamoto ya ukosefu wa vifaa hivi ambavyo  mnakabiliana navyo,’’amesema Kaimu Mkurugezi huyo wa TPA.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za uuguzi  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),  Agness Mtawa ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, amesema  msaada huo utaongeza kasi ya utoaji huduma kwa watoto. Amefafanua kwamba jengo la watoto lina vitanda takribani 300 hivyo mahitaji ya viti vya kubebea wagonjwa pamoja na mahitaji mengine ni makubwa.

“Tunawashukuru TPA kwa msaada huu mliotupatia , mmeongeza kasi ya utoaji huduma niwahakikishie kwamba msaada huu utatumika kama ambavyo imekusudiwa,’’amesema Mkurugenzi Mtawa. Ametoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kuchangia huduma za afya na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma hizo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa (kulia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokea msaada wa viti 20 vya kubebea wagonjwa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bi. Nuru Mhando wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa (kulia) wakiwasukuma watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando (wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa wa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja.


Hivyo makala Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba

yaani makala yote Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/muhimbili-yapokea-msaada-wa-vifaa-tiba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba"

Post a Comment