Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae

Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae
kiungo : Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae

soma pia


Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae

 Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis leo ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na watalaam wake wote kwa jinsi walivyompokea mtoto wake na kumpa huduma stahiki na kwa weledi wa hali ya juu. 
 “Leo natoa shukrani zangu za dhati kwa MNH na kukabidhi barua ya shurakni na cheti cha utambuzi wa huduma nzuri aliyopewa mwanangu Muniri Ali Salim tangu alivyopokelewa kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura na kisha kupelekwa Idara ya Upasuaji Kitengo cha Upasuaji wa watoto. Mtoto wetu alikuwa na uvimbe kichwani ambao ulisababisha afanyiwe upasuaji na kutolewa vizuri, sasa mtoto wetu anaendelea vizuri sana,” amesema Mh. Khamis. 
 Amepongeza kazi nzuri inayofanywa na MNH chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Lawrence Museru kwa kushirikiana na wauguzi, madaktari na watalaam wengine ambao wamekuwa wakijitoa kutoa huduma nzuri kwa mtoto wake pamoja na wahitaji wengine wanaofika MNH kupata huduma.
 “Nimeamua kutoa barua ya shukrani kwenu, cheti cha utambuzi kwa MNH, Idara ya Upasuaji kupitia Kitengo cha Upasuaji Watoto, Idara ya Magonjwa ya Dharura na kipekee kwa Dkt. Juma Mfinanga ambaye ni daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura pamoja na Dkt. Zaitun Bhokare ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji watoto kwa kazi nzuri ambayo imefanikisha matibabu kwa mtoto wetu,” amesema Mh. Khamis. 
 Akipokea cheti na barua kwa niaba ya MNH, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Makwaia Makani amemshukuru Mh. Khamis kwa utambuzi na kutoa mrejesho chanya kutokana na huduma ya matibabu aliyopatiwa mtoto wake. 
 “Sisi kama watoa huduma tunapokea maoni aina zote, lakni maoni ya kupongeza ni machache ukilinganisha na maoni mengine. Hivyo hii imetupa hamasa kubwa sana na watalaam wetu wamefurahi,” amesema Bw. Makani. 
 Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Zaituni Bokhari amesema walimpokea mtoto Munira Ali Salim mwezi mmoja uliopita na baada ya kumfanyia uchunguzi waligundua alikuwa na uvimbe kichwani (kichogoni) na hivyo kumpatia huduma ya upasuaji. 
 Dkt. amesema kuwa baada ya kujiridhisha kwamba ana uvimbe huo kwenye ubongo waliamua kumfanyia upasuaji na kutoa uvimbe huo. Dkt. Bhokari anasema mara baada ya upasuaji mtoto aliendelea vizuri na hatimaye kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Makwaia Makani akipokea cheti cha utambuzi wa huduma zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe- Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis ambaye mtoto wake alipatiwa huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Zaitun Bokhary akipokea cheti cha utambuzi wa huduma kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe- Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Kefa akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya Dkt. Juma Mfinanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
 Wa Pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Makwaia Makani akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Ali Salim Khamis wa Jimbo la Mwanakwerekwe na madaktari wa hospitali hiyo.
 Cheti cha utambuzi wa huduma kilichotolewa kwa hospitali hiyo.
Cheti cha utambuzi alichokabidhiwa Dkt. Zaitun Bokhary.
Cheti cha utambuzi alichokabidhiwa Dkt. Juma Mfinanga.


Hivyo makala Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae

yaani makala yote Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mbunge-wa-mwankwerekwe-zanzibar-mhe-ali.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae"

Post a Comment