MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA

MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA
kiungo : MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA

soma pia


MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA

*Majina ya wanaume waliotelekeza watoto kuanikwa hadharani

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda leo April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.

Ambapo ameeleza  maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda amesema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.

Ameeleza hawapo kwa  ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.Amesema Makonda  ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto  na kuwe na usawa.

Amewataka akina  Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.Makonda ameeleza  Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.

Akizungumza na Michuzi blog Lucy Peter wa Tegeta ameeleza kuwa alitelekezwa mara baada ya kupata ujauzito hadi sasa mtoto wake wa kiume ana miaka 5, na amefika kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa ili baba wa mtoto huyo aweze kutoa huduma mtoto huyo kwani hadi sasa mama huyo anaishi kwa wazazi wake.Aidha Nasra Mohammed ameeleza amefurahi kwa hatua ya Mkuu wa Mkoa ya kuwasaidia wamama waliotelekezwa, hivyo anaamini kuwa mtoto wake atapata huduma stahiki kutoka kwa baba yake aliyemwachia mtoto akiwa na mwezi mmoja.

Hata hivyo wamama hao wamefurahi na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa kuamua kuwasaidia wao na watoto wao hivyo Mungu ambariki sana.Aidha mkuu wa mkoa ameeleza kuwa watahudumia watu 500 kwa siku na maeneo yote nchini hata kama si mkazi wa Dar es salaam kwani ni haki yao na hakuna kuogopau vitisho vya aina yoyote bali waangalie kupata zao za msingi.
Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.
  01.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda  akizungumza na  waliotelekezwa na waume zao juu   kulinda haki za Mama na Mtoto ambapo kama Baba wa watoto   hatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.(Pacha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
 .Mkuu wa Mkoa akizungumza na maofisa mbalimbali wanaotoa huduma na kusisitiza wawasikilize  wakina mama wote hata wale wasio wakazi wa Dar es salaam. .(Pch na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
 Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.



Hivyo makala MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA

yaani makala yote MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mamia-ya-wanawake-waliotelekezwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA"

Post a Comment