title : TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU
kiungo : TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU
TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.
Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.
Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.
"Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.
Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."
Hivyo makala TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU
yaani makala yote TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wao-yasema_22.html
0 Response to "TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU"
Post a Comment