title : Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani
kiungo : Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani
Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Wakili wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba kujitoa kumuwakilisha katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.
Wakati huohuo, mahakama imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha msanii huyo, Wema, katika kesi hiyo na kuomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Desemba 12, mwaka jana katika shauli lililopita mahakama hiyo ilielezwa kuwa wakili wa Wema hajafika na kushindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kuwa amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.
Mbali na Wema, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio, washitakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka jana katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
Hivyo makala Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani
yaani makala yote Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/kesi-ya-wema-kibatala-nje-msando-ndani.html
0 Response to "Kesi ya Wema, Kibatala nje Msando ndani"
Post a Comment