title : RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu
kiungo : RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu
RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando, Kata ya Kirando Wilayani Nkasi.
Amesema kuwa Taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali hiyo.
“Naendelea kuzishukuru taasisi za kidini kwa kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi kwani kwa uopande wa sekta ya Afya Mkoa una zahanati kumi, vituo vya afya vinane na Hospitali mbili zinazomilikiwa na taasisi za kidini na mmeniambia kuwa mnaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya afya ambavyo vikikamilika vitaongeza upatikanaji wa huduma,” Alielezea Mh. Wangabo.
Ametoa mchango huo kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya katika siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Kabwe, Kata ya Kabwe Wilayani Nkasi ambapo Mgeni rasmi wa shughuli hiyo alikuwa Mh. Joachim Wangabo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha katika maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kimkoa Kijiji cha kabwe Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiitikia dua ya kuliombea taifa na serikali ya awamu ya tano, Dua iliyosomwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Shekh Hassan Kiborwa katika maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akiongozana na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga Mh. Adam Mambi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti kuhamasisha upandaji miti kwa waisalamu na wanachi kwa ujumla hasa kipindi hiki cha mvua.
Hivyo makala RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu
yaani makala yote RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/rc-wangabo-achangia-milioni-moja.html
0 Response to "RC Wangabo achangia Milioni Moja kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha Waislamu"
Post a Comment