title : Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa
kiungo : Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa
Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa
Rais wa La Liga Javier Tebas amesema goli alilofunga Messi dhidi ya Valencia jumapili, likakataliwa na refarii lilikuwa ni goli halali ila kutokuwa na teknolojia ya mwamuzi wa video ndio kumesababisha utata huo.
“Nikisema sio goli nitakuwa nadanganya na dunia itaniona muongo na kuniambia labda nimekuwa kipofu, lilikuwa ni goli halali lakini kukosa VAR ndio sababu ya bao hilo kutokukubaliwa”, amesema Tebas.
Tebas amesema msimu ujao matumizi ya Video Assistant Referee (VAR) yataanza bila kuchelewa ili kuepusha makosa kama hayo yaliyotokea kwenye bao la Messi.
Messi alifunga bao halali dakika ya 30 baada ya mkwaju wake kumpita mlinda mlango Neto wa Valencia kabla ya kipa huyo kufanya jitihada za kuuokoa lakini tayari ulikuwa umevuka mstari ila mwamuzi hakuona hivyo kuamuru mechi iendelee.
Barcelona wanaongoza msimamo wa La Liga kwa alama 35 wakifuatiwa na Valencia yenye alama 31. Atletico Madrid ipo nafasi ya 3 ikiwa na alama 27 sawa na mabingwa watetezi Real Madrid wenye alama 27 katika nafasi ya 4.
Hivyo makala Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa
yaani makala yote Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rais-alikubali-goli-la-messi.html
0 Response to "Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa"
Post a Comment