title : KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA
kiungo : KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA
KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa kata za Kigamboni, Vijibweni, Tungi zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika kufuatia kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mgalu aliyasema hayo tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati itahakikisha vituo vingine vya kuboresha hali ya umeme ndani ya jiji la Dar es Salaam vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza.
Aidha, alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha vituo vingine vilivyobaki vya Kurasini, Gongo la Mboto na Mbagala mapema ili wakazi wa jiji la Dar es Salaam waweze kuondokana na tatizo la ukosefu wa umeme.Katika hatua nyingine, Mgalu aliwataka wandarasi waliopewa kazi ya kujenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha miradi mapema na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia mkandarasi atakayezembea ukamilishwaji wa mradi wake.
Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam, Sylvester Sikare (kulia) akielezea maendeleo ya ukamilishaji wa kituo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) mara alipofanya ziara katika kituo hicho tarehe 27 Novemba, 2017.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Richard Swai (kushoto mbele) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) katika ziara hiyo.
Moja ya transfoma zilizopo katika kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA
yaani makala yote KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/kituo-cha-umeme-kigamboni-chakamilika.html
0 Response to "KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA"
Post a Comment