title : KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA
kiungo : KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA
KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA
Mkutano wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance uliokuwa umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Jacaranda ili kuomboleza watu waliouawa na polisi hivi karibuni umesambaratishwa na polisi.
Polisi kuanzia mapema asubuhi walifunga eneo lote la Jacaranda ambako ingefanyika misa hiyo ya kumbukumbu sambamba na tukio la Rais Uhuru Kenyatta kuapishwa kuongoza muhula wa pili wa miaka mitano baada ya kushinda uchaguzi wa marudio Oktoba 26.
Mgombea urais kwa muungano wa Nasa, Raila Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo wa marudio akilalamikia kwamba hayakuwa yamefanyika marekebisho ya kutosha kuwezesha uchaguzi huo kuwa huru na haki.
Baada ya kususia Nasa wamekataa kutambua ushindi wa Uhuru na hawamtambui kama rais wa Kenya. Badala yake leo, wakati Uhuru akiapishwa, alipanga kuwaenzi wafuasi wake waliouawa katika makabiliano na polisi tangu ulipofutwa uchaguzi wa Agosti 8.
Polisi, ambao walikuwa wametangaza kwamba hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi mbali na wa sherehe za kuapishwa Uhuru, wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Nasa waliokuwa wanakusanyika nje ya uwanja huo.
Hivyo makala KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA
yaani makala yote KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/kilicho-mkuta-raila-ondinga-wakati.html
0 Response to "KILICHO MKUTA RAILA ONDINGA WAKATI AKIAPISHWA UHURU KENYATA"
Post a Comment