Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji

Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji
kiungo : Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji

soma pia


Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco , Mhadisi Cyprian Luhemeja akifafanua jambo wakati wa ziara ya kikazi ya bodi mpya ya Dawasco katika mitambo mikubwa ya uzalishaji na usamabazaji Maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu iliyopo Mkoani pwani.

Bodi mpya ya Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), imeridhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika sekta ya Maji ya kuhakikisha kuwa hadi kufikia 2020 tatizo la Maji linakwisha kabisa katika Miji mbalimbali nchini hususani katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kutokana na mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kuwa ya Kisasa na yenye uwezo mkubwa wa kuhudumia mikoa hiyo.

Bodi hiyo mpya ya DAWASCO imeshuhudia uwekezaji mkubwa kwenye miradi hiyo, na kuridhishwa na kazi inayofanywa na shirika hilo mara baada ya kutembelea mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu iliyopo Mlandizi, Pamoja na Bagamoyo Mkoani Pwani, ambapo lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea namna ambavyo serikali imejikita katika kuhakikisha inamaliza tatizo la Maji lililopo nchini na linamtua mama ndoo ya Maji Kichwani.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya DAWASCO, Prof. Tolly Mbwete amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali za kuwekeza katika sekta ya Maji, pia wameridhishwa na kazi kubwa zinazofanywa na DAWASCO pamoja na DAWASA za kuhakikisha wakazi wote wa Dar es salaam na Pwani wanapata huduma bora ya Majisafi hasa wale ambao bado maeneo yao hayajafikiwa na miundombinu ya huduma ya Majisafi.
 "Tumeona kazi kubwa na nzuri inayofanywa na DAWASCO na DAWASA, tumejionea namna ambavyo serikali imewekeza katika sekta hii ya Maji, na namna ambavyo kazi kubwa ya kutibu, kusafisha na kusafirisha Maji inavyofanyika hadi hatua ya kumfikia mlaji, hakika sio kazi nyepesi, inahitaji nguvu na kujituma zaidi ili watu wote waweze kupata huduma bora” alisema Prof. Mbwete. Pia, wajumbe wengine wa bodi hiyo,Wamefurahishwa na namna ambavyo taasisi hizo zinavyofanya kazi ya uzalishaji na utibuji Maji kwa ufanisi na utaalamu wa hali ya juu.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema kuwa ziara ya bodi ya DAWASCO imekuja wakati mwafaka ambapo Shirika hilo lipo katika kupambana pamoja na kumaliza tatizo la upotevu wa Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani. Aidha, ameeleza kuwa maeneo mengi ambayo yalikuwa na changamoto ya huduma ya Majisafi kwa sasa yanapata huduma hiyo, hasa katika maeneo ambayo yapo pembezoni mwa barabara ya Morogoro kuanzia Mbezi, Kimara, Ubungo pamoja na maeneo mengi ya Tabata kwa sasa wanapata huduma ya Majisafi, hasa baada ya kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.

“Mitambo hii ya Ruvu juu na Chini ina hudumia sehemu kubwa ya Jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Pwani, hivyo kutokana na upanuzi uliofanyika katika mitambo hii maeneo mengi sasa yanapata huduma Majisafi ya kutosha na hata yale maeneo yaliyokuwa na changamoto kutokana na miinuko, sasa yanapata huduma”. alisema Mhandisi Luhemeja.

Bodi ya DAWASCO iliyozinduliwa mapema na Mh Waziri wa Maji ,Mh Isack Kamwele mapema wiki hii imekuwa ni bodi ya Tano tangu shirika hilo kuanza majukumu yake ya kuzalisha na kusambaza Maji katika Mkoa wa Dar es salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani pwani ambapo itakuwa chini ya Mwenyekiti wake Profesa Tolly Mbwete..


Hivyo makala Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji

yaani makala yote Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/bodi-ya-dawasco-yaridhishwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji"

Post a Comment