title : BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA.
kiungo : BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA.
BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA.
ikiwa benki ya Exim ina Mradi unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali hapa nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.Mashuhuda wa msaada huo unavyotolewa ni Mwenyekiti wa bodi wa hospitali Dodoma
Job Lusinde na Daktari mkuu wa Mkoa wa Caroline Damian.
Daktari wa Mkoa wa Dodoma,Caroline Damian akizungumza mara baada ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma kupokea msaada wa Vitanda na magodoro 40 za hospitali za Mkoa hou ikiwa Exim Bank Tanzania ikiwa kwenye mradi wa kupunguza upungufu wa vitanda na magodoro katika hospitali za hapa nchini.
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania mara baada ya kukabidhi magodoro na vitanda 40 katka hospitali za mkoa wa Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge akisikiliza kwa makini
HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma.
Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka huu, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania. Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Bilinith Satano Mahenge alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya rufaa ya Dodoma.
Hivyo makala BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA.
yaani makala yote BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/benki-ya-exim-yakabiliana-na-upungufu.html
0 Response to "BENKI YA EXIM YAKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE MA HOSPITALI NCHI NZIMA."
Post a Comment