title : TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA
kiungo : TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA
TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA
Mahakama nchini imeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli zake mbalimbali, ambapo kwa siku mbili mfululizo mashauri tofauti yalisikilizwa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video (Video Conference). Katika shauri la kwanza, Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara ilisikikila kesi namba 80 ya mwaka 2015 kwa kutumia teknolojia hii, ambapo shahidi muhimu katika shauri hili aliunganishwa kutoka nchini Kanada. Na katika shauri jingine, Mahakama Kuu ilisikiliza kesi ya madai (Civil Case) namba 225 ya mwaka 2013 ambapo shahidi wa kesi hii alikua nchini Uswisi (Switzerland), na mahakama zilihamia kwa muda kwenye kumbi za mikutano kwa njia ya video za Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).
Mawakili wa Pande Zote Kabla ya Kesi Kuanza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti majaji wanaosikiliza kesi hizi wamesema teknolojia hii itawezesha kusikilizwa kwa mashahidi na hatimae kumalizwa kwa mashauri hayo na mengine ambayo ni ya muda mrefu.
Mawakili Kutoka NL and Partners Advocates (Mlalamikaji) Kabla ya Kesi Kuanza.
Teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video, ni teknolojia inayowezesha washiriki kutoka vituo viwili au zaidi kuwasiliana kwa kuonana (video) na kusikilizana. Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imekua ikitoa huduma hizi tangu mwaka 2000 ambapo teknolojia hii imekua ikitumika kwa shughuli mbalimbali kama mikutano ya kawaida, kusikilizwa kwa kesi mbalimbali, usaili, uwasilisho wa miradi na maandiko, midahalo, mafunzo, kuonana na madakrari bingwa, n.k.
Hivyo makala TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA
yaani makala yote TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/teknolojia-ya-mawasiliano-kwa-njia-ya.html
0 Response to "TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO YATUMIKA KUSIKILIZA MASHAURI YA KIMAHAKAMA"
Post a Comment