PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA

PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA
kiungo : PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA

soma pia


PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA

Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wametoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutoa huduma bora zinazoendana na viwango vya kimataifa .

Wakizungumza hii leo katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, baadhi ya wateja waliofika ofisini hapo kupata huduma mbalimbali wamesema weledi na uharaka wa kupata huduma toka kwa wafanyakazi wa Mfuko huo ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine nchini.

Jessica Mmasy ni miongoni mwa wanachama waliofika kupata huduma hii amesema upotevu wa muda wa kungoja huduma katika ofisi mbalimbali imekuwa kikwazo kikubwa nchini lakini PPF wamepata suluhisho la changamoto hiyo.

“Nimehudumiwa ndani ya dakika tano tu, kitu ambacho ni sehemu chache unaweza kukuta hivyo wanatoa huduma kwa makini wapo ‘professional’(weledi) na wanajali muda wa mteja,”

amesema mteja huyo ambae alifika ofisini hapo kupata huduma. Naye Mustafa Adamu ambaye ni mwanachama wa PPF amesema mfumo wa utoaji huduma katika ofisi za PPF unatoa nafasi kwa kila mwanachama kuhudumiwa kwa usawa na bila manungúniko.

“Hapa ukifika wa kwanza,utakuwa wa kwanza kuondoka pia,kuna mfumo maalumu wa kuhudumiwa kutokana na namba unayopewa hivyo hakuna kugombania kwenda kwenye dirisha la mhudumu,” alifafanua mteja huyo.

Kwa upande wake meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko huo Michael Christina amesema wameienzi wiki ya huduma kwa wateja kama sehemu ya utendaji wao wa kazi wa kila siku.

“Tumepata cheti cha kutoa huduma kwa kiwango cha kimataifa (ISO 900: 2015 certified) hivyo kutoa huduma bora ni jadi yetu kila siku katika utekelezaji wa majukumu yetu”,amesema meneja huyo.
Meneja Uhusianao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akimwelezea huduma zinatolewa na Mfuko huo mwanachama wa PPF Mustafa Adamu (kulia) alipofika katika ofisi za Mfuko huo kupata huduma.
Mwanachama wa PPF Wiliam Dagharo (Kushoto) akisisitiza jambo kwa mtoa huduma wa PPF katika ofisi za Mfuko wa PPF Makao Makuu jijini Dar es Salaam hii leo.
Mwanachama wa Mfuko wa PPF Bi.Mkemwema Said (kulia) akipata huduma katika ofisi za PPF jijini Dar es Salaam hii leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Michael Christian (Kushoto) akitoa huduma kwa mwanachama wa PPF Jessica Mmasy (kulia) aliyefika katika ofisi za PPF Makao Makuu jijini Dar es Salaam tarehe 6/10/2017 katika kilele cha wiki ya huduma wateja.
Wateja mbalimbali wakipata huduma katika ofisi za Mfuko wa Pensheni za PPF hii leo jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA

yaani makala yote PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/ppf-yapongezwa-kwa-huduma-bora.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PPF YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA"

Post a Comment