title : MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'
kiungo : MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'
MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa.
Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti.
Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa. Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani.
“Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
Uzinduzi unaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.
Hivyo makala MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'
yaani makala yote MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA' Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA' mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/mkuu-wa-mkoa-wa-shinyanga-azindua.html
0 Response to "MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'"
Post a Comment