title : Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000.
kiungo : Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000.
Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000.
Kamati ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu kwa Mkoa wa Dar es Salaam imepokea msaada wa matofali 1000 kutoka kwa kampuni ya A and Bel Impex Tanzania Limited kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu wilaya ya Kigamboni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu amesema wanaipongeza kampuni hiyo kwa kujitolea msaada huo huku akieleza kuwa utasaidia katika kuboresha elimu kwa ujenzi wa ofisi za walimu kwani katika shule 513 za Mkoa wa Dar es Salaam asilimia kubwa ya takribani shule zaidi ya 400 hazina ofisi za walimu jambo ambalo ni changamoto katika maendeleo ya elimu.
Lissu amesema kuwa ujenzi wa ofisi 402 za walimu kwa mkoa wa Dar es Salaam utakamilika kwa muda wa miaka miwili ila utakuwa na awamu katika shule za kila wilaya ambapo ameelekeza matofali hayo 1000 yapelekwe shule ya Nguva Sekondari ya Wilaya hiyo ya Kigamboni na ujenzi uanze mara moja kuanzia hivi sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya A and Bel Impex Tanzania Limited iliyotoa msaada wa matofali hayo bwana Thobias Hima ameeleza kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu na watahakikisha pale panapohitajika msaada wanafanya hivyo kwa maendeleo ya watanzania wote.
"Licha ya kutoa matofali haya 1000 tumetoa pia na mashine ya kufyatulia matofali na eneo la kufanyia shughuli hiyo la Mwembe Mdogo, Mtaa wa Minondo Kata ya Somangila" Alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Kanali Charles Mbuge ameeleza kuwa ufyatuaji wa matofali utakuwa unafanyika majira ya usiku katika eneo hila la kata ya Somangila, huku akihimiza wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika kufikia lengo la ujenzi wa ofisi hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni David Mgonja ameeleza kuwa shule zitakazo pitiwa na mpango huo ni 12 na zitakuwa kwa awamu huku 4 zikiwa za sekondari na 8 za msingi, ambapo awamu ya kwanza itajumuisha shule mbili za sekondari na tatu za msingi, za sekondari zikiwa Nguva na Tungi, huku za msingi ni Mwongozo, Mizimbini na Vumilia Ukooni.
Hivyo makala Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000.
yaani makala yote Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/kampuni-ya-and-bel-impex-ya-unga-mkono.html
0 Response to "Kampuni ya, A and Bel Impex ya Unga mkono ujenzi ofisi za Walimu Dar yachangia matofali 1000."
Post a Comment