IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA
kiungo : IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

soma pia


IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.

Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.

“Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

yaani makala yote IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/imarisheni-takwimu-za-ujenzi-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA"

Post a Comment