title : WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo.
kiungo : WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo.
WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo.
Mkurugenzi mtendaji wa WAJIBU alipokuwa akizungumza kuhusiana na ripoti iliyotolewa ambayo imezinduliwa leo.
Hawa ni wadau walioshirki katika uzinduzi huo wa ripoti ya uwajibikaji katika taasisi hiyo.
Mgeni rasmi Dr. Annette Mummert (katikati) wakati akizindua ripoti ya tatu ya uwajibikaji katika mashirika ya Umma, Serikali kuu pamoja na serikali za mtaa.
Na Noel Rukanuga
Mwambawahabari
Taasisi WAJIBU (Institute of Public Accountability) imefanikiwa kuzindua ripoti tatu za uwajibikaji katika Mashirika ya Umma, Serikali Kuu pamoja Serikali za mtaa.
Ripoti hizo zimetokana na uchambuzi uliofanya kupita ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16 ya Mashirika ya Umma na kuweza kutoa mapendekezo katika uwajibikaji.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hizo Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU Ludovick Utouh, amesema kuwa ripoti hiyo imelenga kutoa mapendezo juu ya hatau ambazo zinapaswa kuchuliwa na serikali.
Amesema kuwa wamepitia ripoti hiyo ya CAG yenye ukurasa zaidi ya 400 ili kuhakikisha wanatoa mapendekezo bora ambayo yanaweza kuwa chachu ya maendeleo kwa serikali ya Tanzania.
Utouh ameeleza kuwa katika ripoti hiyo wamajaribu kupendekeza masuala mabalimbali ambapo kama serikali wakifanyia kazi taifa la Tanzania linaweza kuwa na maendeleo katika masula ya kiuchumi.
Amebainisha kuwa miongoni mwa athari zinazoweza kujitokeza hasa kwa kutokulipwa kwa kodi kunaathiri kiasi cha mapato ambayo Serikali ingepata.
Hata hivyo sehemu ya mapendekezo katika ripoti hizo imeonyesha kuwa Menejimenti za taasisi hizo zinashauriwa kuchukua hatua stahiki za kisheria ili kuhakikisha makato yote ya kisheria yanapelekwa kwenye taasisi husika kwa wakati. Kwani kufanya hivyo itasaidia kuepuka faini, riba na adhabu zisizokuwa za lazima.
WAJIBU ni taasisi fikra ya uwajibikaji wa Ummailiyoanzishwa mwaka 2015 kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kukuza uwajibikaji na Utawala bora hapa nchini.
Kwa lengo la kukamilisha adhma hiyo, WAJIBU kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16 ya Mashirika ya Umma imeandaa Ripoti ya Uwajibikaji katika Mashirika ya Umma. Mashirika ya Umma kisheria ni mashirika ambayo Serikali inaumiliki wa kuanzia asilimia 50.
Hivyo makala WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo.
yaani makala yote WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/wajibu-wazindua-ripoti-ya-mwaka-201516.html
0 Response to "WAJIBU wazindua ripoti ya mwaka 2015/16, Wafanya uchambuzi wa CAG, Watoa mapendekezo."
Post a Comment