title : SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA
kiungo : SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA
SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA
Mwambawahabari
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibadilishana nyaraka za mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakitia saini karatasi ya makubaliano ya udhamini wa timu ya Singida wenye thamani ya Milioni 250.
Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United Festo Sanga akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexande Macedo wakionesha mfano wa jezi ambao utatumiwa na timu ya Singida United.
Kocha Mkuu wa klabu ya Singida Hans Van Der Pluijm akiongea na waandishi wa habari baada ya Kampuni ya YARA kuingia mkataba na klabu hiyo wenye thamani ya shilingi milioni 250.
Wachezaji wa Singida United wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexande Macedo (kulia) Kocha Mkuu wa Singida United Hans Van Der Pluijm (kushoto)
Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United Festo Sanga wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
…………………………………
Wageni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Timu ya Singida United imezidi kupata Neema ya Udhamini baada ya leo kuingia mkataba wa mwaka mmoja ukiwa na thamani ya kiasi cha Milioni 250 na Kampuni ya Uzalishaji mbolea ya YARA ikiwa ni ishara ya kujimalisha katika upatikanaji wa vyanzo vya mapato ya timu hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari katika uwekaji wa saini Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Singida United Festo Sanga amesema kuwa kupata udhamini huu wa mwaka mmoja utasaidia katika kuimarisha morali kwa wachezaji kwani masuaala ya kifedha yatakuwa yameongezeka na huku akizidi kukaribisha zaidi makapuni mengine kwa ajili ya kupata udhamini mwingine.
Hata hivyo Sanga amesema kuwa,mbali ya kupata udhamini huo pia kuna makubaliano ya kuanzisha Kilimo cha Mahindi na tayari wameshapata shamba la Ekari 10000 na shughuri hizo za kilimo zitasimamiwa na Kampuni ya YARA ikiwemo uwekezaji wa mazao hayo ndani ya nje ya nchi.
Sanga alisema kwamba YARA Tanzania kwa kipindi hiki ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwani thamani yake ya udhamini ni kubwa kuliko wadhamini wengine hata hivyo wamekubaliana kufanya biashara ya kusambaza bidhaa za YARA ndani ya nchi kwa kuzitangaza.
Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya YARA,Alexander Maced amesema kuwa wameamua kuidhamini timu ya Singida United kwani wameiona kuwa ni bora kwao na ukizingatia hata nembo yao ina Ua la Alizeti ambalo linatumika kwa ajili ya utengenezaji wa mafuta hayo na Mkoa wa Singida ni mmoja wapo wanaofanya biashara ya zao hilo.
Mkurugenzi huyu Maced ambaye anatoka nchini Brazil amesema kuwa watashirikiana na klabu ya Singida United kwa kuwezesha kuimarisha na kuendeleza kilimo cha Mahindi nchini pamoja na kuhakikisha kuwa wanaleta wataalamu wazuri katika kuendeleza soka kwa kutoa mafunzo zaidi na kwa vitendo.
Hivyo makala SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA
yaani makala yote SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/singida-united-yazidi-kunenepa-na.html
0 Response to "SINGIDA UNITED YAZIDI KUNENEPA NA UDHAMINI, YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA YARA"
Post a Comment