title : OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO
kiungo : OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO
OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO
Na Woinde Shizza,Arusha
Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa na chama hicho.
Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyeji
Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa katika uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010.
Alisema kuwa yeye binafsi hajawaona watu hao wanaodaiwa ni Waganga wa kienyeji na usahili ulienda vizuri katika kipindi hiki uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .
“Nasema kwakweli ili suala na mgombea wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona, ila ukweli napenda kuchukua nafasi hii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuita kikao kama jambo ni gumu sana, pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dkt Dallo.
Alizitaja baadhi ya kanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na nyingi
Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobaki.
Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi
Hivyo makala OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO
yaani makala yote OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/ole-wake-mgombea-atakae-enda-kinyume-na.html
0 Response to "OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO"
Post a Comment