MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR
kiungo : MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

soma pia


MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR


Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano lilodumu kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi wao nchini Tanzania.

Akihutubia mamia ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.

Alisema kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.

Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.

Alisema kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya utambuzi wao.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufungaKongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara. (Picha zote na Mathias Canal)
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddykatika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.



Hivyo makala MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

yaani makala yote MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_27.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR"

Post a Comment