title : Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao.
kiungo : Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao.
Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao.
Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Jang’ombe Boys Khamis Mussa “Rais”, Ahmed Ali wa Jamhuri pamoja na Mwalimu Mohd wa Jamhuri wao ndio vinara wa kupachika mabao kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora inayoendelea katika mzunguko wake wa sita.
Washambuliaji hao mpaka sasa wameshafunga jumla ya mabao 4 kila mmoja katika michezo mitano waliyocheza.
Wengine wanaofuatia ni Ibrahim Hamad “Hilika” wa Zimamoto, Khamis Said wa JKU, Nassor Matar wa JKU, Nabil Mohammed wa Okapi, Seif Saleh wa Okapi, Abdull Yussuf wa Mwenge, Salim Mussa wa Mwenge, Khatib Hassan wa Kizimbani, Nassir Suleiman wa Kizimbani, Mussa Ali wa Jamhuri na Hassan Haji wa Zimamoto wote hao wana mabao 2.
Hakim Khamis “Men” ndie Mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ulopita alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa msimu huo.
Hivyo makala Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao.
yaani makala yote Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/wachezaji-wa-ligi-kuu-nane-bora.html
0 Response to "Wachezaji wa Ligi Kuu Nane Bora Wafukuzana Kwa Kufunga Mabao."
Post a Comment