title : Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi
kiungo : Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi
Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi
Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia siku ya Jumamosi ya tarehe 15 July 2017 katika jiji la London. Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa.
Viongozi waliochaguliwa ni: Dada Lynne Kimaro (Mwenyekiti), Ndg. Omwami George Ndibalema (Makamu Mwenyekiti), Ndg. Lazaro Matiku (Katibu), Dada Halima Yusuph (Naibu katibu), na Dada Edith Kimaro (Mweka Hazina)
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & NI, kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae.
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK
Asanteni,
Uongozi Tanzania Diaspora Community/Association
United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland
Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa (wa pili kulia) akiwa na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa London
Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania London Dada Lynne Kimaro
Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akiwa katikia picha ya pamoja na wanachama na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania London. Picha kwa hisani ya TZUK
Hivyo makala Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi
yaani makala yote Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/jumuiya-ya-watanzania-wa-london.html
0 Response to "Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi"
Post a Comment