title : ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA
kiungo : ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA
ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA
MASHINDANO ya ligi ya kombe la Diwani wa kata Saranda, Tarafa ya Kilimatinde, wilayani Manyoni, Mkoani Singida yamefikia tamati kwa timu ya soka ya ILALOO FC kuwa mabingwa wa kombe hilo kwa mwaka huu wa 2017 baada ya kuifunga timu ya Saranda FC kwa jumla ya magoli 2-1.
Ligi hiyo iliyoanza kuchezwa juni, 29 mwaka huu kwa makundi mawili yaliyokuwa yakivitumia viwanja vya michezo vya Shirika la reli Tanzania (TRC) ilizishirikisha jumla ya timu sita za kata hiyo ambazo ni pamoja na Saranda FC, Ilaloo FC, Irucha, Mlimani A, Mlimani B na Mhegahega FC.
Akitangaza matokeo ya mashindano hayo, Katibu wa Chama Cha mpira wa miguu wilaya ya Manyoni (MADIFA), Joshua Msemakweli aliwataka vijana hao kuwekeza kwenye mchezo wa soka kwa kuamini kwamba michezo ni afya na michezo ni ajira.
“Mashindano ngazi ta kata ya Saranda yalishirikisha timu sita kutoka katika vijiji na vitongoji,ambavyo ni Kijiji cha Saranda ambapo ndipo makao makuu ya kata pia Ilaloo na Irucha zipo Kijiji cha Saranda Kijiji cha Saranda kilikuwa na timu tatu”alifafanua Msemakweli.
Kwa upande wake muandaaji wa kombe hilo ambaye pia ni diwani wa kata ya Saranda,Joseph Ndahani aliyataja baadhi ya malengo ya michezo hiyo kuwa ni kuhakikisha wanakuza pamoja na kuvitangaza vipaji wa vijana wa kata hiyo kupitia sekta ya michezo.
Naye Mwalimu wa timu ya soka ya Ilaloo FC ambao ndiyo mabingwa wa kombe hilo, Rashid Juma alikishukuru kituo hiki kwa kuweza kufika katika Kata hiyo na kuwawezesha kusikika maana haijawahi kutokea bahati kama hiyo kwa vituo vingine kufika huko.
Katibu wa Chama Cha Mpira wa miguu wilaya ya Manyoni (MADIFA) Joshua Msemakweli (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa timu pamoja na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa fainali katika kata ya Sanjaranda.
Hivyo makala ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA
yaani makala yote ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/ilaloo-fc-mabingwa-kombe-la-diwani.html
0 Response to "ILALOO FC MABINGWA KOMBE LA DIWANI SARANDA"
Post a Comment