title : WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA
kiungo : WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA
WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA
*Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar
*Yabainika kuwa inafaa kwa matumizi ya kilimo
*Asisitiza wakulima waanze kupulizia mikorosho
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema salfa iliyoingizwa nchini kwenye makontena 211 haina kasoro na inafaa kwa matumizi ya kupulizia kwenye mikorosho.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 10, 2017) wakati akizungumza na wajumbe wa kamati maalum, waagizaji wa salfa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) kwenye kikao alichokiitisha kwenye makazi yake, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
“Bodi kaandaeni taratibu za kawaida kusambaza salfa kwa wakulima ili waanze kupuliza dawa hiyo. Wasichelewe kupuliza kwa sababu msimu umeshaanza,” amesema.
Juni 4, mwaka huu Waziri Mkuu alimuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samuel Manyele aende kuchunguza mzigo wa salfa ulioko bandari ya Dar es Salaam baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ripoti ya TPRI kuwa ya salfa iliyoingizwa nchini na kampuni ya ETG Inputs Ltd kwa niaba ya Bodi ya Korosho haijakidhi viwango.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa salfa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt Mathew Mtigumwe. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali , Samwel Manyele (kulia) ya chunguzi wa Salfa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Mathew Mtigumwe. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Hivyo makala WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA
yaani makala yote WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/waziri-mkuu-apokea-taarifa-ya-uchunguzi.html
0 Response to "WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA"
Post a Comment