title : BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
kiungo : BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Baraza la Wazee Jijini Arusha wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwaangalia wazee ambao walikuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii mambo mazuri bali manufaa wameyakosa baada ya kuvunjika Jumuiya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa Baraza hilo Mathius Kichao amesema kuwa hadi sasa kuna wazee ambao hawajalipwa stahiki zao jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwani wazee hao wananung'unika
"Kuna muda wazee hawa waliandamana wakenda Dar es salaam ,wakalala barabarani,lakini viongozi wawakati ule hawakuona umuhimu kuwa kilio cha wazee ni hatari sana wakawafukuzwa,nitamke kuwa hadi sasa kuna wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa chochote kile, niikumbushe Serikali wale wazee wanalaani ,naomba hii laana isitokee,Mhe,Magufuli awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii vizuri zaidi "alisema Mwenyekiti huyo
Aidha wazee hao katika jiji la Arusha wameiomba serikali ya awamu ya tano ipeleke mswada wa wazee katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na upitishwe ili Wazee nchini Tanzania waweze kunufaika na matunda ya nchi yao kwani wao ni chombo cha harakati hivyo Taifa likiwasahau wazee hakuna maendeleo kwasababu wazee huwa wanafahamu mambo mengi ya kihistotia ya Nchi pamoja na mila nzuri na desturi.
"Tunawaomba viongozi mbalimbali wa Taifa hili wanapotembelea mkoa wa Arusha watenge muda wao ili waweze kuonana na wazee tutawashauri kwa yale tunayoyafahamu kwaajili ya manufaa ya nchi yetu na watoto pamoja na wajukuu zetu.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee mkoa wa Arusha Mathius Kichao aliyeshika karatasi mkononi,akiwa anazungumza na waandishi wa habari hivi katibuni Jijini hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa wazee wa Baraza la wazee Jijini Arusha Kassim Seremuka akizungumza jinsi ambavyo wazee hao wamenifaika na vitambulisho vya bima ya afya .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Baraza la wazee katika mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja .Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa Baraza la wazee Kassim Seremuka Jiji la Arusha akionyesha Kadi ya matibabu wanazotumia wazee wakienda kutibi wa Hospitalini.
Hivyo makala BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/baraza-la-wazee-jijini-arusha-wamuomba.html
0 Response to "BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment