OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI

OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI
kiungo : OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI

soma pia


OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI



Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar yazinduliwa rasmi.

Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar zilizinduliwa rams tarehe 19 Mei 2017. Shughuli za ufunguzi ziliongozwa na Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar ambaye alisaini kitabu cha wageni kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Ubalozi.


Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Watanzaia wanaoishi nchi Qatar walishiriki katika hafla hiyo.

Mhe. Balozi alitumia fursa hiyo kuzungumza machache na Watanzania walioshiriki. Aliwaeleza kwamba kufunguliwa kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar ni sehemu ya kutekeleza malengo ya Serikali ya Tanzania ya kusogeza huduma zake kwenda kuwekeza Tanzania hususan katika sekta ya viwanda. Aliwahakikishia kwamba Ubalozi utawapatia ushirikiano watakaouhitaji katika kufanikisha azma hiyo.

Balozi aliwapongeza Watanzania hao kwa kuendelea kuwa na sifa nzuri nchini Qatar na kudumisha mshikamano miongoni mwao. Aliwahimiza waendelee kuwa raia wema na kulinda haiba na jina la Tanzania kwa kufuata sheria za nchi wanapoishi. Alisema milango ya Ubalozi itakuwa wazi kupokea ushauri wao katika mambo ambayo yatalenga kuleta tija na mafanikio kwa taifa. 

Naye Bw. Said Ahmed, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Qatar aliishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na hatimaye kufungua Ubalozi na kuwa na Balozi Mkazi nchini Qatar. Alimueleza Balozi kwamba jamii ya Watanzania wanaoishi Qatar itashirikiana na Ofisi za Ubalozi na kufanya kazi bega kwa bega katika kuitafutia maslahi Tanzania. Wawakilishi hao waliomba Ubalozi uandae mkutano mkubwa utakaowawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki ili kusikia maoni yao na changamoto zinazowakabili. Balozi aliahidi kufanya mkutano huo mapema iwezekanavyo. 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Doha, Qatar 24 Mei, 2017 .
Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Qatar akiongea na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar 
Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar 


Hivyo makala OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI

yaani makala yote OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/ofisi-ya-ubalozi-wa-tanzania-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI"

Post a Comment