title : MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI
kiungo : MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI
MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI
Nimesikitishwa sana na kifo cha Ivan, ni mapema sana kwa yeye kuondoka duniani kuacha watoto wadogo sana, wanahitaji sana uwepo wa baba na mama, lakini Mungu ni Mwema amependezwa nae kuwa karibu yake mbinguni.
Naweza kusema nimekufahamu baada ya kuwa na mpenzi wako Diamond, umeonyesha msimamo na uimara wako ambao ni ushahidi mzuri kuwa utawatunza wanao watatu ambao sasa wako mikononi mwako forever. Usikate tamaa wengi tumepitia uliyopitia, kuvunjika kwa ndoa na kufiwa na wenzetu na kubakia na watoto, yalinikuta mimi binafsi hayo sikujua ada, nauli, kusomesha watoto hadi mwenzangu alipofariki mwaka 1994 nikiwa Idara ya elimu ya juu na mshahara wa ualimu, na watoto kurudi kwangu, hapo ndio niliona jinsi Mungu huongeza baraka zake, na jinsi ukoo wa Kamota ulivyosimama nami kulea watoto.
Na wewe daima muweke Mungu mbele mambo yatakuwa mazuri, hasa ukizingatia ulishajiimarisha na baba watoto wako amewaacha vizuri. Mungu atakuongezea na kukutia furaha ya maisha ya familia yako, na bila kusahau kuwa Diamond yuko pemebeni yako, tabasamu lake linatosha kukuongezea amani na nguvu ya maisha na kilo za uzito wa mwili confidence!
Diamond amelelewa vizuri sana na mama yake na yuko wazi katika penzi lenu, sasa ni wakati wa kushikamana kikamilfu kupeana raha na amani na kuijenga familia yenu .
Kila la heri Zari, huenda tukaonana JHB maana sehemu ya maisha yangu ni JHB kwa mume wangu Orange Grove na Alexander township!
GOD BLESS YOU AND YOUR FAMILY ZARI
MAMA BISHANGA / MRS MAROLEN
CLEVELAND. OHIO
Hivyo makala MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI
yaani makala yote MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mama-bishanga-amlilia-ivan-x-husband-wa.html
0 Response to "MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI"
Post a Comment