title : WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE
kiungo : WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE
WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE


Sehemu ya kiwanda cha kuzalisha vinywaji baridi jamii ya Cocacola ,kiwanda cha Bonite Ltd mjini Moshi.





Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
ZAIDI ya wateja 15,000 wa vinywaji baridi vinavyozalishwa na kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mjini Moshi wamejishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya “Coke Studio kunywa na Ushinde “ inayoendelea .
Wateja hao wamejishindia zawadi baada ya kununua soda jamii ya Cocacola ,Fanta na Sprite zikiwa katika ujazo wa mililita 350 na mililita 500 huku wengine 22 wakikabidhiziwa zawadi zao za Televisheni za kisasa za ukubwa wa inchi 32.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao kutoka mikoa ya ,Arusha,Kilimanjaro na Manyara imefanyika katika viunga vya Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd na baadae washindi wote walipata nafasi ya kutembelea na kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za Bonite.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Boniface Mwase alisema wateja wa bidhaa zinazozalishwa na Bonite kila mmoja yupo kwenye nafasi ya kujishindia zawadi kwa kutumia kiasi cha Sh 500 na sh 1000.
“Zawadi ambazo tumezitoa leo (Jana) ni televisheni 22 kwa washindi ambao wamejitokeza ,zipo zawadi za soda za bure ,zipo zawadi za fedha kiasi cha sh 5000 hadi 10,000,hizi zinatolewa pamoja hapo mteja anapokunywa soda anashinda papo hapo “alisema Mwase.
Alisema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye shindano la Coke Studio kunywa na ushinde na washindi wameendelea kupatikana kutoka maeneo yote ambayo bidhaa za Bonite zinapatikana na kwamba kila atakayeshinda atafikishiwa zawadi yake kwa wakati.
Mwase alisema Bonite imekuwa na utaratibu wa kufanya Promosheni kila mara lengo likiwa ni kurejesha seheu ya faida inayopata kwa wateja ambao wamekuwa wakiunga mkono kampuni hiyo kwa kutumia bidhaa zake.
“Nitoe wito kwa wateja wetu waendelee kutumia soda za jamii ya Coca Cola kwa sababu zawadi bado ni nyingi na kila mmoja ana nafasi ya kushinda.”alisema Mwase.
Zainaabu Lusoke ,mkazi wa Arusha ni mmoja wa washindi wa Televisheni katika promoshen ya Coke Studio kunywa na ushinde amesema zawadi hiyo inatokana na Mama yake mdogo aliyemtaka kuokota kizibo alichotupa pindi aliponunua Soda aina ya Fanta.
“Katika shindano hili sikutegemea kama nitashinda ,nilinunua soda nikatupa kile kizibo ,ma mdogo akaniambia kwa nini unatupa ,nikamwambia hivi vizibo vya Bonite vimeandikwa Jaribu tena ,akaniambia kachukue kile kizibo ,ndipo nilipotizama nikakuta nimeshinda TV”alisema Zainabu.
Washindi waliojinyakulia zawadi za Televisheni ni pamoja na Mariam Mkara,Saumu Rashid ,Hadija Mmbughu,Emanuel Magige,Lightnes Lusega,Mwanahawa Miraji,Mohamed Hussein na Fadhili Lyimo.
Wengine ni Hilda Silayo,Judith Assey ,Haruna Mohamed,Nasibu Juma,Happy Kombe,Fii Mkwanda,Emanuel John,Nembris Simon,Godfrey Wilson ,Zainabu Salim,Rajabu Miraji,Said Massatu na Laurant Mlingi.
Mwisho.
Hivyo makala WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE
yaani makala yote WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/watu-elfu-15-wajinyakulia-zawadi-katika.html
0 Response to "WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE"
Post a Comment