title : MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA
kiungo : MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA
MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MASHEIKH wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( BAKWATA) katika mikoa yote ya Tanzania wamempongeza Sheikh Mkuu Aboubakary Zubeiry kutokanana namna ambavyo amejenga umoja na mshikamano ndani ya baraza hilo.
Wametoa kauli hiyo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 ya BAKWATA tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968.Akizungumza kwa niaba ya masheikh wa mikoa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema wanampongeza wanampongeza Muft Zubeiry kwa namna ambavyo amefanya mabadiliko makubwa ya kuwaunganisha Waislamu nchini.
"Wakati leo tunasheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa BAKWATA ,salamu za kipekee tunazipeleka kwa Mufti wa Tanzania kwani maadhimisho hayo yanamkuta yakiwa mikononi mwake."Chini ya Mufti wetu Sheikh Zubeiry BAKWATA imekuwa mpya,na walio chini yake tunapendana,tunaheshimiana na tunajitambua .Kupitia kauli mbiu yake ya Jitambue, Mabadilaka,Acha mazoea hakika imetusaidia kutubadilisha na kila mmoja wetu anajua majukumu yake," amesema Sheikh Alhad.
Amesisitiza kupitia Mufti wa Tanzania BAKWATA imeunganishwa na walio chini yake wamekuwa waaminifu na walio tayari kuhakikisha baraza hilo linasonga mbele kimaendeleo.Pia amesema kuwa BAKWATA kwa sasa wamekuwa na uhusiano mzuri na taasisi nyingine na chini ya Mufti Zubeiry kuna maendeleo makubwa yanaendelea kufanyika ukiwamo wa ujenzi wa msikiti mkubwa ambao unajengwa katika makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA
yaani makala yote MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/masheikh-wa-bakwata-mikoa-yote-nchini.html
0 Response to "MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA"
Post a Comment