TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAARIFA KWA UMMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAARIFA KWA UMMA
kiungo : TAARIFA KWA UMMA

soma pia


TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
 
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ndugu January Makamba (Mb), leo anaanza ziara ya mikoa 19 nchini, ambayo itafanyika kwa awamu tatu. Ziara hiyo inamadhumuni yafuatayo:- 

1. Kukagua, kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi wa mikoa husika kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira. 

Kama inavyofahamika, Sheria ya Mazingira, hasa vifungu vya 47, 51, 54, 56, na 58 (3), inatoa mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya mazingira kutangaza, kutamka au kuamuru, kupita kwenye Gazeti la Serikali, baadhi ya maeneo nchini kuwa ni Maeneo Lindwa Kimazingira (Environmental Protected Area) au Maeneo Nyeti Kimazingira (Environmental Sensitive Area). 


Nyenzo hizi zimewekwa ili kuyalinda maeneo muhimu kwa mifumo ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa, mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki, misitu, nk.) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine. Sheria imeweka vigezo kwa maeneo hayo.

 Ofisi ya Makamu wa Rais, kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), iliomba na kupokea kutoka katika Halmashauri mbalimbali nchini mapendekezo ya maeneo hayo. Jumla ya maeneo 77 yalipendekezwa, ikiwemo vyanzo muhimu vya maji, mazalia ya samaki na wanyama adimu, maeneo ya ardhi oevu, mabwawa, mito na chemichemi nyeti. Mikoa iliorodhesha maeneo hayo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Sheria. Katika awamu ya kwanza, maeneo takriban 20 yanatarajiwa kuhifadhiwa kwa kutumia Sheria ya Mazingira. 

Katika ziara yake, Ndugu Makamba anatarajia kuyaona maeneo hayo, kutathmini hoja na haja ya kuyahifadhi na kuzungumza na viongozi wa mikoa, halmashauri na wananchi katika maeneo hayo ilikubaini utayari na uwezo wao katika kusimamia uhifadhi mara maeneo hayo yatakapotangazwa. Vilevile, katika ziara hiyo, Ndugu Makamba atapokea mapendekezo ya maeneo mapya hasa pale ambapo mapendekezo yaliyotolewa awali hayakutokana na ushirikishwaji mpana. Orodha ya maeneo yanayopendekezwa itatolewa kadri ziara inavyoendelea katika kila mkoa. 




Hivyo makala TAARIFA KWA UMMA

yaani makala yote TAARIFA KWA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KWA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/taarifa-kwa-umma.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TAARIFA KWA UMMA"

Post a Comment