title : VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI
kiungo : VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI
VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini , Baba Askofu Dkt Martin Shao amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo itayoshughulika na kutatua kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji.
Kwa kuanza taasisi hiyo imepanga kuanza matengenezo ya barabara katika vijiji vyote Vilivyoko katika Jimbo la Vunjo ,barabara ambazo zinakadiliwa kuwa na urefu wa Km 272.8 ambazo zitagharimu kiasi cha Sh Bil 7 na Mil 290.Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo uliofanyika katika kata ya Mshiri ,Marangu wilaya ya Moshi ,Katibu wa Bodi ya taasisi hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia amesema Vunjo litakuwa jimbo la kwanza kufanya tukio hilo.
“Mzigo huu tulionao utakuwa mwepesi tukiw ana raha kwenye nafsi zetu ,na tunataka tuongoze kama wana vunjo hili liwe jimbo la kwanza Tanzania kwa watu wake kuwa na raha bila ya kuwa na bughdha za aina yoyote”alisema Mbatia.Alisema tukio la kuleta viongozi wa Dini pamoja ,viongozi wa vyama vya siasa pamoja na ananchi pamoja kufanya na kukubaliana kwa maendeleo yao na kwamba litakuwa ni jimbo la mfano kwa majimbo mengine kwa kuanzisha utaratibu huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo,Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dkt Martin Shao alisema taasisi hiyo bado ni changa lakini hata hivyo tayari imeweza kuanza kazi kwa upande wa miundombinu ya barabara.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akikata utepe katika mtambo unaotumika kukarabati barabara ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa Taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza barabara katika jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akibariki moja ya Mitambo itakayotumika katika kufanya matengenezo ya barabara katika jimbo la Vunjo.

Mtambo wa kukwangua barabara ukianza kazi muda mfupi baada ya kuzinduliw kwa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza miundo mbinu ya barabara.
Hivyo makala VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI
yaani makala yote VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/vunjo-wazindua-taasisi-yao.html
0 Response to "VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI"
Post a Comment